Ufunuo wa Yohana 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 3 (Swahili) Revelation 3 (English)

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. Ufunuo wa Yohana 3:1

"And to the angel of the assembly in Sardis write: He who has the seven Spirits of God, and the seven stars says these things: "I know your works, that you have a reputation of being alive, but you are dead.

Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu. Ufunuo wa Yohana 3:2

Wake up, and keep the things that remain, which you were about to throw away, for I have found no works of yours perfected before my God.

Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako. Ufunuo wa Yohana 3:3

Remember therefore how you have received and heard. Keep it, and repent. If therefore you won't watch, I will come as a thief, and you won't know what hour I will come upon you.

Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. Ufunuo wa Yohana 3:4

Nevertheless you have a few names in Sardis that did not defile their garments. They will walk with me in white, for they are worthy.

Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake. Ufunuo wa Yohana 3:5

He who overcomes will be arrayed in white garments, and I will in no way blot his name out of the book of life, and I will confess his name before my Father, and before his angels.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Ufunuo wa Yohana 3:6

He who has an ear, let him hear what the Spirit says to the assemblies.

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. Ufunuo wa Yohana 3:7

"To the angel of the assembly in Philadelphia write: "He who is holy, he who is true, he who has the key of David, he who opens and no one can shut, and who shuts and no one opens, says these things:

Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu. Ufunuo wa Yohana 3:8

"I know your works (behold, I have set before you an open door, which no one can shut), that you have a little power, and kept my word, and didn't deny my name.

Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda. Ufunuo wa Yohana 3:9

Behold, I give of the synagogue of Satan, of those who say they are Jews, and they are not, but lie. Behold, I will make them to come and worship before your feet, and to know that I have loved you.

Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Ufunuo wa Yohana 3:10

Because you kept my command to endure, I also will keep you from the hour of testing, which is to come on the whole world, to test those who dwell on the earth.

Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. Ufunuo wa Yohana 3:11

I am coming quickly! Hold firmly that which you have, so that no one takes your crown.

Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. Ufunuo wa Yohana 3:12

He who overcomes, I will make him a pillar in the temple of my God, and he will go out from there no more. I will write on him the name of my God, and the name of the city of my God, the new Jerusalem, which comes down out of heaven from my God, and my own new name.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Ufunuo wa Yohana 3:13

He who has an ear, let him hear what the Spirit says to the assemblies.

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. Ufunuo wa Yohana 3:14

"To the angel of the assembly in Laodicea write: "The Amen, the Faithful and True Witness, the Head of God's creation, says these things:

Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Ufunuo wa Yohana 3:15

"I know your works, that you are neither cold nor hot. I wish you were cold or hot.

Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Ufunuo wa Yohana 3:16

So, because you are lukewarm, and neither hot nor cold, I will vomit you out of my mouth.

Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Ufunuo wa Yohana 3:17

Because you say, 'I am rich, and have gotten riches, and have need of nothing;' and don't know that you are the wretched one, miserable, poor, blind, and naked;

Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. Ufunuo wa Yohana 3:18

I counsel you to buy from me gold refined by fire, that you may become rich; and white garments, that you may clothe yourself, and that the shame of your nakedness may not be revealed; and eye salve to anoint your eyes, that you may see.

Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Ufunuo wa Yohana 3:19

As many as I love, I reprove and chasten. Be zealous therefore, and repent.

Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Ufunuo wa Yohana 3:20

Behold, I stand at the door and knock. If anyone hears my voice and opens the door, then I will come in to him, and will dine with him, and he with me.

Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Ufunuo wa Yohana 3:21

He who overcomes, I will give to him to sit down with me on my throne, as I also overcame, and sat down with my Father on his throne.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Ufunuo wa Yohana 3:22

He who has an ear, let him hear what the Spirit says to the assemblies."